Kizaa zaa Tena Shinyanga!! KABURI LA MAREHEMU ALIYEZIKWA NA KUKU TUMBONI ,LAFUKULIWA,MIGUU YA WATU NA FISI YAKUTWA KABURINI

Kaburi la marehemu Benadetha Steven aliyefariki dunia hivi karibuni kutokana na uvimbe tumboni aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga aliyezikwa na kifaranga cha kuku tumboni na ndugu zake kwa madai kuwa wanaondoa mikosi katika familia.Pichani ni kaburi lake likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana-Picha na Kadama Malunde
 Kaburi la marehemu Benadetha limekutwa limefukuliwa huku sanda na jeneza likiwa linaonekana na alama za  nyayo za miguu ya watu na miguu ya mnyama aina ya fisi zikionekana katika kaburi hilo.Inasemekana kuna watu walionekana eneo la makaburi juzi wakiwa na gari na inadaiwa udongo umepelea kaburini pengine umechukuliwa na watu hao wasiojulikana-Picha na Kadama Malunde

Wananchi wakiwa kaburini ambapo walisikika wakisema :“Tunalaani kitendo hiki,tumekuta jeneza na  sanda ya marehemu inaonekana,hiki kitendo kimefanywa na binadamu tu maana kaburi lilikuwa refu sana,fisi hawezi kufukua,hapa kuna alama za miguu ya watu na fisi,fisi  atakuwa amesikia harufu ya maiti,na fisi hawezi kuingia kwenye shimo,binadamu wamekosa utu”-Picha na Kadama Malunde

Wananchi wakiwa katika eneo la kaburi la marehemu kabla ya kuzika tena-Picha na Kadama Malunde

Mkuu wa upelelezi jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Musa Athuman Taibu(mwenye suti) akiwa kwenye kaburi la marehemu ambapo alisema jeshi la polisi halina mamlaka ya kufukua kaburi la marehemu bali mahakama pekee ndiyo yenye yenye mamlaka ya kutoa kibali cha kaburi kufukuliwa hivyo kuwaomba wananchi kufukia kaburi hilo badala ya kulifukua.

Benadetha Steven(35) alikuwa anaishi mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala,alifariki dunia Januari 1,2015,wakati akitibiwa uvimbe wa tumboni katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kuzikwa katika makaburi ya Masekelo ambapo mazishi yake yalileta utata baada ya ndugu wa marehemu kutoka mkoani Mara(Wakurya) kuingia kaburini na kuchana tumbo la marehemu kwa wembe kisha kuchinja kifaranga cha kuku kwa wembe na kuingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu.
Picha na Kadama Malunde
 

ANGALIA PICHA NYINGI ZAIDI NA HABARI HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post