WAREMBO ZAIDI YA 20 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUUZA MIILI YAO


Watu 22 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya jiji la Dar es salaam kwa makosa mawili tofauti,likiwemo la kufanya biashara ya kuuza miili yao.

Akisoma shtaka hilo mwedesha mashtaka Ramadhan Kalinga alisema watuhumiwa hao walikamatwa maeneo ya Ubungo na kwamba walikuwa wakiuza miili yao huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.


Washtakiwa walikana na kurudishwa RUMANDE kutimiza masharti ya dhamana na shauri lao litaendelea tena Januari 13 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post