Inadaiwa kuwa Moshi alichukua uamuzi huo baada ya Alphonce kumdhulumu zaidi ya Sh87.4 milioni.
Wakizungumza na gazeti hili jana, watu wa karibu
na wafanyabiashara hao ambao hawakupenda majina yao kuandikwa kwenye
gazeti, walidai kuwa wafanyabiashara hao walikuwa wakiishi nyumba ya
ndugu yake, Didas na kufanya biashara za kuuza mbao pamoja.
Walidai kuwa, Desemba 30 mwaka jana,
wafanyabiashara hao walikuwa wakinywa pombe kwenye Bwalo la Magereza na
Moshi alikuwa akilalamika kudhulumiwa na Didas.
Mashuhuda hao waliongeza kuwa tangu siku hiyo, wafanyabiashara hao hawakuonekana tena hadi jana.
Ilidaiwa kuwa, mwenye nyumba huyo alitumia funguo
zake za akiba kufungua nyumba hiyo na kukuta mwili wa mjomba wake ukiwa
umepigwa na shoka na tayari umeanza kuharibika.
Mtu mmoja ambaye jina lake tunalihifadhi alitoa
taarifa kituo cha polisi na walipofika waliubaini pia mwili wa Moshi
aliyejinyonga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai uchunguzi wa awali
unaonyesha wafanyabiashara hao walikuwa wanadaiana pesa.
Alisema Mosha ameacha ujumbe mrefu wa karatasi nne aliouandika kuhusiana na mauaji hayo.
Ujumbe huo: “Kataeni wadhulumaji kati ya matajiri
na maskini, nimeondoa dhambi kubwa ya dhuluma iliyokuwa ikinitesa
ulimwenguni, wadhulumaji wasifumbiwe macho jamii iniunge mkono kuondoa
watu hawa. “Dhuluma aliyonifanyia mtu huyu imekatisha maisha yangu.”
Social Plugin