MTOTO WA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA KENYA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA KITANDANI
Sunday, January 04, 2015
Prezzo akiwa na Fidel Odinga katikati na marafiki wengine
Simanzi kubwa imeikumba familia ya waziri mkuu wa zamani wa Kenya
Raila Amolo Odinga baada ya kutoka kwa taarifa ya kifo cha mtoto mkubwa
wa mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Kenya asubuhi ya leo .
Mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Fidel Odinga alikutwa akiwa
amefariki dunia kitandani kwake asubuhi ya leo (jumapili) baada ya
kurudi nyumbani kwake alfajiri akiwa anatoka kukutana na rafiki zake .
Mara ya mwisho Fidel aliripotiwa kukutana na baba yake usiku wa
jumamosi kabla ya kuagana na kwenda kukutana na rafiki zake katika
sehemu ambayo haijawekwa wazi na baada ya hapo alirudi nyumbani
kupumzika hadi mauti yalipomkumba .
Fidel Odinga
Mwili wa Fidel Odinga ulikutwa kitandani kwake baada ya kurudi nyumbani alfajiri akiwa anatoka kukutana na rafiki zake .
Hadi mauti yanamkumba Fidel Odinga alikuwa na umri wa miaka 42 na
Polisi nchini Kenya wameanza uchunguzi wa kifo cha mtoto huyo wa
mwanasiasa maarufu nchini Kenya huku bado kukiwa hakuna taarifa zozote
kuhusiana na chanzo cha kifo chake .
Aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga.
Fidel ameacha mke mmoja na mtoto mmoja mwenye umri wa miaka miwili
ambaye alizaa na mke wake Getachew Bekele ambaye ni raia wa Eritrea .
Fidel Odinga siku alipofunga ndoa na mkewe Getachew Bekele.
Saa chache baada ya habari za kifo cha Fidel makundi tofauti ya watu
yalianza kufanya maandamano na vurugu maeneo ya Ngong nje kidogo ya Jiji
la Nairobi wakipiga kelele za ‘Nani amemuua Fidel’ wakimaanisha kuwa
kifo chake kimesababishwa na mtu huku wakishindwa kutaja sababu au
chanzo kamili .
Social Plugin