Ukatili wa kijinsia unaendelea kutikisa Mkoa wa Mara ambapo mwanamke
mmoja Rhobi Mwita amelazwa katika hospitali teule ya Mkoa ya Bunda baada
ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa kuingizwa chuma sehemu za siri na
mume wake Mwita Chacha kutokana na wivu wa mapenzi.
Akisimulia mkasa huo akiwa hospitalini,mwanamke huyo alisema siku
hiyo mumewe ambaye alikuwa amelala kwa mke mkubwa alifika nyumbani na
kumkuta akiwa anakamua ng’ombe maziwa.
“Baada ya kufika nyumbani alimuuliza binti yetu niko wapi,alipoambiwa
ninakamua ng’ombe alinifuata na kuanza kunigombeza kuwa usiku wa siku
hiyo niliingiza mwanaume na kufanya nae tendo la ndoa,nilijitetea
sijafanya hivyo lakini akaanza kunishambilia kwa kipigo na kuninyonga
shigo kwa kutumia kitenge hadi nikaanguka na kupoteza fahamu”alisema
mwanamke huyo.
“Nilipozinduka nikajikuta mimi na binti yetu wa miaka 13 tumefungwa
mikono huku nikiwa na chuma aina ya nondo sehemu za siri,baadaye
akatufungulia na kuanza kutupiga tena kabla ya kutokomea.
Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo Ester Maduhu alisema mwanamke
huyo alipokelewa akiwa na hali mbaya na kwamba kwa sasa hali yake
inaendelea vizuri.
Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka
Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951
Social Plugin