Noma Kweli!!! AFISA MTENDAJI ASHUSHIWA KIPIGO CHA MAANA BAADA YA KUCHAKACHUA MATOKEO YA UCHAGUZI HUKO KILIMANJARO


Wananchi wa kijiji cha Nduoni kata ya kirua vunjo  magharibi  mkoani Kilimanjaro  wamefunga ofisi ya kijiji  na kumpiga afisa mtendaji wa kata hiyo kwa madai ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi uliopita  kwa  kumtangaza mgombea wa chama cha mapinduzi kuwa mshindi badala ya mgombea wa chama cha NCCR mageuzi.

Wananchi hao walikusanyaika katika ofisi ya kijiji hicho wakiwa na mabango mbalimbali  na kusema kuwa wanasikitishwa na hatua ya serikali kumwapisha mgombea wa chama cha mapinduzi Bw.Joseph  Msaki aliyepata kura 158 na kumwacha mgombea wa chama cha NCCR mageuzi Bw.Thomas Ngowi aliyechaguliwa na wananchi kwa kupata  kura 163.
Wamesema wamefikia hatua ya kufunga ofisi hiyo kwa madai ya kupewa kiongozi ambaye siyo chaguo la wananchi kwa kuwa serikali ilimwapisha kwa nguvu  mgombea wa chamacha mapinduzi kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho 
Kufuatia vurugu za wananchi hao  afisa mtendaji wa kata ya kirua vunjo magharibi bw.reginald mlay alilazimika kumtangaza  rasmi Bw.Thomas kupitia tiketi ya chama cha NCCR mageuzi kuwa ndiye mshindi halali wa kijiji hicho baada ya kupata kura 163 akifuatiwa na mgombea cha chamacha mapinduzi aliyepata kura 158 na tlp kura tisa
Naye mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha NCCR mageuzi taifa  Bw.Hemed Msabaha  amesema mtendaji huyo alikiuka kanunu za uchaguzi  kwa kuhujumu maamuzi ya wapiga kura jambo ambalo limesababisha vurugu ambazo zinatishia usalama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post