PAPA FRANCIS ATEUA MAKADINALI 20,MAJINA YOTE YAPO HAPA

 
Papa Francis (PICHANI)amewachagua makadinali 20 wapya akiwemo kutoka mataifa ya Tonga,Ethiopia na Myanmar.


Kumi na tano kati yao wako chini ya umri wa miaka 80 swala linalowafanya kuingia katika mkutano faragha ili kumchagua atalkayemrithi papa.

Papa Francis amesema kuwa uteuzi wa makadinali hao kutoka mataifa 14 kutoka kila bara duniani unaonyesha kuwa uhusiano wa karibu wa Vatican na makanisa ya kikatoliki kote duniani.
Makadinali hao wataapishwa rasmi tarehe 14 mwezi February.

Papa Francis pia alitangaza kuwa siku ya jumapili kwamba ataongoza wa makadinali wote ili kujadiliana kuhusu usimamizi wa kanisa hilo huko Vatican mnamo tarehe 12,13 februari.
Makadinali hao wapya ni:
Manuel Jose Macario do Nascimento Clemente (portugal)
Berhaneyesus Demerew Souraphiel (Ethiopia)
John Atcherley Dew (New Zealand)
Edoardo Menichelli (Italy)
Pierre Nguyen Van Nhon (Vietnam)
Alberto Suarez Inda (Mexico)
Charles Maung Bo (Myanmar)
Francis Xavier Kriengsak Kovithavanij (Thailand)
Francesco Montenegro (Italy).
Daniel Fernando Sturla Berhouet (Uruguay)
Ricardo Blazquez Perez (Spain).
Luis Lacunza Maestrojuan (Panama)
Arlindo Gomes Furtado, (Capo Verde).
Soane Patita Paini Mafia (Tonga)
Jose de Jesus Pimiento Rodríguez (Colombia)*
Luigi De Magistris (Italy)*
Karl-Joseph Rauber (Germany)*
Luis Hector Villalba (Argentina)*
Julio Duarte Langa (Mozambique)

Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post