Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA_ JINSI DIWANI WA CHADEMA ALIVYOCHEZEA KICHAPO LEO MJINI SHINYANGA

Diwani wa kata ya Ndala George Sungura katika manispaa ya Shinyanga Sungura akiwa ameshikilia mti wakati vijana wa CCM wilaya ya Shinyanga waliokuwa hawajavaa sare za Chama wakimshambulia leo asubuhi.Katikati ni Suzana Nicholaus anayedaiwa kuongoza vijana wa CCM kumwadhibu diwani wa Ndala,inaelezwa kuwa diwani huyo kapigwa vibao,kutukanwa kisha kusukumwa barabarani na kunusurika kugongwa na gari lililokuwa katika mwendokasi,lakini bahati nzuri akadakwa na msamaria mwema aliyekuwa karibu na barabara hiyo ili karibu na ofisi za CCM.
 Diwani huyo amejikuta katika wakati mgumu baada ya kupita katika ofisi za CCM wilaya akitokea kwenye ofisi za afya za manispaa ya Shinyanga zilizopo jirani na jengo hilo la CCM,ambapo ghafla vijana hao waliokuwa wamefunga ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini wakishinikiza viongozi wa ngazi ya wilaya waondolewe madarakani kutokana na kuonekana kusaliti CCM na kufanya ishindwe katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika manispaa ya Shinyanga walipomvamia na kuanza kumshambulia wakidai hawataki viongozi wa upinzani wapite hapo kwani huwa wanaiba siri za CCM-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

 
Diwani wa CHADEMA George Sungura akisukumwa barabarani -picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Msamaria mwema aliyeokoa maisha ya diwani wa CHADEMA-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog










Diwani wa Kata ya Ndala George Sungura akizungumza katika moja ya mikutano ya CHADEMA mwaka 2014-Picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog.Kufuatia tukio hilo diwani huyo amesema anafungua kesi polisi kutokana na kitendo hicho cha kudhalilishwa mbele ya umma.Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Tajiri Maulid amesema CCM itawachukulia hatua za kidhamu vijana hao.
SOMA ZAIDI HAPA 

 Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka  
"HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com