TAZAMA PICHA- TUKIO KUBWA LILILOFANYWA NA MAASKARI POLISI WA SHINYANGA USIKU

Kulia ni mshereheshaji mkuu wa sherehe ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kuaga mwaka 2014 na kukaribisha mwaka 2015 iliyokwenda sambamba na kuwaaga askari wake wawili wanaobadili vituo vyao vya kazi na kuwapatia zawadi wafanyakazi 20 bora wa jeshi hilo katika mwaka 2014,katika ukumbi wa bwalo la polisi mjini Shinyanga.Kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya sherehe Pili Misungwi-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga

Ufunguaji Shampeni unaendelea

Wageni mbalimbali wakiwa eneo la tukio

 Cheeers

 Meza imependeza
 Kulia ni Mgeni rasmi Annarose Nyamubi,kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha(katikati) na mwenyekiti wa kamati ya sherehe Pili Misungwi kabla ya kukata keki wakati wa sherehe hizo usiku wa kuamkia jana 
Mgeni rasmi Annarose Nyamubi akimlisha keki kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha wakati wa sherehe hizo usiku wa kuamkia jana 
 Askari wawili waliaagwa wakiwa na wake zao-Kushoto ni mnadhimu 2 mkoa wa Shinyanga Peter Nduguru anayekwenda kuwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbulu mkoani Manyara na mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Deusderis Rugimbana(Aliyeshikilia kipaza sauti) anayekwenda kuwa mkuu wa usalama barabarani mkoa wa kipolisi Ilala jijini Dar es salaam.Pichani wakijiandaa kukata keki
 Sherehe inaendelea
 Ukumbi ulipendeza kweli kweli
 Wengine walijitokeza kucheza muziki
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi akizungumza katika sherehe hiyo ambapo aliwataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama hususani katika kipindi hiki taifa likielekea kufanya matukio makubwa mawili ya kupigia kura katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa mwaka huu.


Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema pamoja na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la polisi ni vyema wananchi wakashirikiana na polisi ili kuhakikisha kuwa amani inaendelea kuwepo katika jamii.
 Waandishi wa habari walikuwepo eneo la tukio 
 Usiku wa kuaga mwaka 2014,kukaribisha mwaka 2015,kuaga maafisa wawili wa jeshi la polisi Shinyanga na kupongeza maafisa 20 waliofanya kazi nzuri mwaka 2014
 Kila mmoja anajimwaga kivyakeeee
 Meza zilipendeza haswaaaa
.
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi (wa pili kutoka kushoto) aliyekuwa mgeni rasmi akicheza muziki na wageni waalikwa mbalimbali
Burudani ilichukua nafasi yake-Picha zote na Na Kadama Malunde-Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi amewataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama hususani katika kipindi hiki taifa likielekea kufanya matukio makubwa mawili ya kupigia kura katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Nyamubi ameyasema hayo usiku wa kuamkia jana Jumapili wakati wa sherehe ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kuaga mwaka 2014 na kukaribisha mwaka 2015 iliyokwenda sambamba na kuwaaga askari wake wawili wanaobadili vituo vyao vya kazi na kuwapatia zawadi wafanyakazi 20 bora wa jeshi hilo katika mwaka 2014.

Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema pamoja na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la polisi ni vyema wananchi wakashirikiana na polisi ili kuhakikisha kuwa amani inaendelea kuwepo katika jamii.

“Kila kwenye mafanikio ya polisi,nyuma yake kuna raia mwema aliyetoa taarifa,tunaomba ushirikiano uliopo udumu hususani katika matukio ya kitaifa yanayokuja,hakuna haja ya kuogopa polisi wananchi toeni taarifa zitakazosaidia kuondoa uhalifu katika jamii,pia tushirikiane katika kupiga vita ukatili wa kijinsia”,alisema Nyamubi.

Aidha alilipongeza jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kazi nzuri na iliyotukuka wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 kwani Shinyanga ni miongoni mwa mikoa michache nchini ambako uchaguzi ulikamilika kwa utulivu hapakuwa na matukio makubwa ya kutisha.

“Tumejifunza mengi katika uchaguzi wa serikali za mitaa,sasa tunajipanga vyema kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao ili uwe wa amani na utulivu,lakini yote haya yatawezekana kama kutakuwepo ushirikiano wa wadau mbalimbali”,aliongeza Nyamubi.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alisema changamoto iliyopo ni upungufu wa askari polisi kwa sababu hivi sasa askari mmoja analazimika kuhudumia wananchi 1584 wakati inatakiwa ahudumie wananchi 350 hadi 500 hivyo ushirikiano unahitajika zaidi ili kufanya Shinyanga kuwa mahali salama pa kuishi binadamu.

Kamanda Kamugisha alisema nidhamu inaendelea kuporomoka kila siku hivyo kuwataka askari wake kuendelea kuwa na nidhamu nzuri kwani nidhamu ndiyo msingi mzuri wa kusimamia sheria.

“Mwaka 2014 haki ya nidhamu katika jeshi letu ilikuwa nzuri,japokuwa askari 7 walifukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu na wengine 6 kubadilishwa vituo vya kazi,hii inaonesha kiasi gani tulivyo makini na suala la nidhamu kwani huduma yetu inagusa watu wengi,askari mmoja akionesha utovu wa nidhamu anachafua jeshi la polisi na serikali iliyoko madarakani”,aliongeza Kamugisha.

Katika Sherehe hizo za kuaga mwaka 2014 na kukaribisha mwaka 2015 zilizojulikana kama “Polisi Family Day” jumla ya wafanyakazi wa polisi mkoa wa Shinyanga walitunukiwa zawadi kwa kazi nzuri waliyoifanya katika jeshi la polisi mwaka 2014.

Aidha askari wawili waliagwa ambao ni afisa mnadhimu 2 mkoa wa Shinyanga Peter Nduguru anayekwenda kuwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbulu mkoani Manyara na mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Deusderis Rugimbana anayekwenda kuwa mkuu wa usalama barabarani mkoa wa kipolisi Ilala jijini Dar es salaam.

Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post