Tukio la Kutisha!! AGONGWA NA TRENI HUKO MOROGORO,VIUNGO VYA MWILI VYASAMBAA,KICHWA CHAPOTEA

Mtu mmoja ambaye  hakuweza kufahamika mara moja amegongwa na TRENI katika eneo la Kingolwira  nje kidogo ya mji wa Morogoro  na viungo vya mwili  kusambaa  zaidi ya mita mia moja.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia askari na wananchi wakiokota vipande vya viungo vya mwili  ikiwemo miguu na mikono  na hawakufanikiwa kukipata kichwa  ingawa viungo vingine  kama  miguu mikono   kifua vilipatikana.
Wananchi wa eneo la Kingolwira wamesema   huenda mtu huyo  alikuwa  mlevi  alikuwa anavuka  reli usiku bila kuchukua tahadhari
 Station master  mkoa wa Morogoro  Flavian  Nyawale   amesema    wamekabidhi  jeshi la polisi tukio  hilo  ili kufanya uchunguzi na kutoa tahadhari kwa wananchi watembea kwa miguu  kuach akutembea kando kando  ya reli na kuchukua tahadhari wakati w akuvuka  katika makutano ya reli na barabara ili kuepusha matukio ya ajali  zisizo za lazima.
Kamanda wa reli  Enginea Simon Chillery  akizungumza  kwa njia ya simu akiwa njiani kuelekea nachingwea amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo  na amesema mtu huyo ambaye hakufahamika jina lake  anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 na 40  na uchunguzi  wa tukio hilo unaendelea na kuwakumbusha wananchi kuheshimu sheria za reli kama ilivyo sheria za barabarani  kwa watembea kwa miguu  na wanaendesha vyombo vya moto wanapovuka reli.
via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post