VPL>>HAYA HAPA MATOKEO YA MECHI ZA LEO,YANGA,AZAM,SIMBA NA MBEYA CITY

Mpira ukigonga mwamba kwenye lango la Ruvu Shooting, kufuatia kona ya Andrey Coitinho (hayupo pichani)  kuunganishwa kwa kichwa na Simon Msuva Kwenye mchezo wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara 2014/2015 leo Januari 17.

  Yanga SC imepata sare ya pili mfululizo baada ya kumaliza dakika 90 dhidi ya Ruvu Shooting bila bao.

Sare hiyo inakuwa ni ya pili kwa Kocha Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi ambaye amerejea kuinoa Yanga.

Katika mechi hiyo ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Yanga ilipoteza zaidi ya nafasi tatu za kufunga kupitia Simon Msuva, Amissi Tambwe na Andrey Couinho.
Kocha Goran Kopunovic ameanza Ligi Kuu Bara vizuri baada ya kuiwezesha Simba SC kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

Simba SC imeshinda mechi hiyo ikiwa ugenini leo Januari 17,2015 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Vijana hao wa Msimbazi walifunga bao kila kipindi wakianza kupitia kwa Danny Sserunkuma aliyeonekana kufanya vizuri katika mechi hiyo ambapo Kipindi cha pili, Simba SC ilikianza vizuri na harakaharaka ilifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Elius Maguli.

Huu ni ushindi wa pili kwa Simba SC  tokea ilipoifunga Ruvu Shooting mwishoni mwa mwaka jana 2014 ,ukiwa ni ushindi pekee chini ya Patrick Phiri halafu ikatoka sare mechi sita na kupoteza moja dhidi ya Kagera Sugar.


Hapa  Kambarage,Mkoani  Shinyanga, Azam FC wameifunga Stand United Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 43 la Frank Domayo na kukaa kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 1 mbele ya Mtibwa Sugar ambao wanacheza Jumapili januari 18,2015 Ugenini na JKT Ruvu.

Huko CCM Kirumba, Mwanza, Mbeya City wameifunga Kagera Sugar, wanaotumia Uwanja huo kwa Mechi za Nyumbani baada Kaitaba kufungwa kwa ukarabati, Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 80 la Peter Mapunda.

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post