VURUGU KUMPINGA RAIS ZATOKEA,WANAFUNZI WAPIGWA MABOMU

 
Waandamanaji wakichoma matairi ya magari

Rais Kabila amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001
Polisi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, wamefyatua risasi hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika mji mkuu Kinshasa kupinga sheria mpya ya uchaguzi.

Serikali inasema kuwa watu wanne walifariki katika vurugu za Jumatatu ingawa upinzani unasema idadi huo huenda ikawa juu kuliko iliyonakiliwa.

Wanafunzi wameweka vizuizi barabarani na pia wameshuhudiwa wakichoma magurudumu, katika barabara zinazoelekea katika chuo kikuu mjini humo.

Wanatuhumu wanasiasa wanaomuunga mkono Rais Joseph Kabila ambaye muhula wake wa pili unatarajiwa kumalizika mwaka ujao kwa kujaribu kujiongeza muda mamlakani kwa kuidhinisha mipango ya kufanyika sensa ambayo itachelewesha uchaguzi kwa miaka mingi.

Vurugu hizi zinashuhudiwa huku baraza la Senate likidadisi mswada ambao huenda ukasababisha Rais Kabila kuongezwa muda mamlakani.

Vijana walioandamana kwa vurugu, waliteketeza magurudumu ya magari, kupora maduka na kurusha mawe.

Wanafunzi waliambia BBC kuwa polisi walivamia chuo chao baada ya wao kuanza kuandamana.

Walisema polisi waliingia katika vyumba vyao na kuwafyatulia gesi ya kutoa machozi.

Viongozi wa upinzani walitoa wito kwa waandamanaji kwenda barabarani kupinga mipango ya serikali kumuongeza muda zaidi mamlakani Rais Joseph Kabila huku wakiutaja mpango huo kuwa mapinduzi ya kikatiba. 

Mswada huo unapendekeza kufanyika sensa kote nchini ambayo itachukua kipindi cha miaka mitatu.

Rais Kabila amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001. Muhula wake wa pili unakamilika mwaka 2016 kikatiba. 
via>>BBC
 
Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara tu Tunapozitoa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post