WANANCHI WAUA KWA KUMPIGA MAWE JAMAA ALIYEIBA NG'OMBE WATATU HUKO SHINYANGA VIJIJINI

 
Mwanamme aitwaye jina Paul Luhende(38) ameuawa kwa  kupigwa mawe fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu kuiba ng’ombe watatu katika kijiji na kata ya Mwakitolyo wilaya ya Shinyanga vijijini mkoani Shinyanga.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha tukio hilo limetokea Januari 6,mwaka huu  saa nane mchana.


Alisema wananchi hao waliojichukulia sheria mkononi walimuua mtu huyo kwa kumpiga mawe na fimbo baada ya kumtuhumu kuiba ng’ombe watatu wenye thamani ya shilingi 1,200,000/=,mali ya Subi Khamis(48) mkazi wa Mwakitolyo.


Kamanda Kamugisha alisema chanzo cha tukio hilo ni wananchi kujichukulia sheria mkononi na kwamba juhudi za jeshi la polisi kuwabaini na kuwakamata wahusika wa tukio hilo zinaendelea.
Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post