Mwanamke
mmoja mkazi wa kata ya Buhare katika manispaa ya Musoma mkoani Mara
Bi.Helena Paulo mwenye umri wa miaka 20 amejifungua watoto wawili
mapacha ambao wameungana katika eneo la kifua hadi tumboni tukio
ambalo limevuta mamia ya wananchi ambao wamefika katika Hospitali ya
rufaa mkoa wa Mara mjini Musoma kwa lengo la kutaka kushuhudia tukio
hilo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo ya
rufaa ya mkoa wa mara mjini ,Musoma,muuguzi wa zamu Bi. Naabu
Geraruma,amesema kuwa mwanamke huyo amefanikwa kujifungua usiku wa
saa saba kuamkia leo Jumatatu kwa njia ya operesheni watoto hao wawili wenye jinsi ya
kike huku wakiwa na uzito wa kilo
4.6
Hata hivyo muuguzi huyo wa zamu amesema tukio hilo ni la kwanza
kutokea katika Hospitali ya mkoa wa Mara na kwamba hali za mwanamke
huyo na watoto zinaendelea vema na taratibu za kumpeleka hospitali ya
rufaa ya Bugando jijini Mwanza zimekamika.
Hata hivyo mkurugenzi wa utawala na rasmali watu wa hospitali ya
rufaa ya Bugando Bi.Leah Kagine amesema tayari mwanamke huyo na
watoto wamefikishwa katika hospitali ya rufaa kwa ajili ya matibabu
na uchunguzi zaidi.
Social Plugin