ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUMTIA VIDOLE SEHEMU ZA SIRI MTOTO WA MIAKA MINNE


MKAZI wa Bangulo Hali ya Hewa, Baraka Benson (30) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es salaam akikabiliwa na mashitaka ya kumnajisi mtoto wa miaka minne.
 
Benson alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma.
 
Wakili wa Serikali, Florida Wenslaus alidai kwamba Desemba 23 mwaka jana, maeneo ya Bangulo Hali ya Hewa Wilaya ya Ilala, Benson alimnajisi mtoto huyo wa miaka minne kwa kumtia vidole sehemu za siri huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
 
Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande kwa kushindwa masharti ya dhamana.
 
 Awali, wakili Wenslaus alidai kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali.
 
Hakimu Juma alimtaka mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja kutoka taasisi inayotambulika, watakaosaini dhamana ya Sh milioni mbili.
Kesi itasikilizwa maelezo ya awali Machi 3 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post