ANGALIA PICHA - KERO MJINI SHINYANGA

Hii ni barabara ya Magadula  inayotoka eneo la Hospitali ya mkoa wa Shinyanga hadi Mshikamano (kata ya Ndembezi na Ngokolo)mjini Shinyanga ambapo vifusi vya mchanga vimemwagwa kipindi kirefu bila kusambazwa matokeo yake barabara inakuwa finyu hali inasababisha waendesha magari,pikipiki,mikokoteni,baiskeli na watembea kwa miguu kupita kwa tabu kama inavyoonekana pichani
Kutosambazwa huko kwa vifusi kumesababisha magari kuharibu hata mitaro pembezoni mwa barabara

Watumiaji wa barabara hiyo walipozungumza na Malunde1 blog mbali na kuulalamikia uongozi wa  manispaa ya Shinyanga kwa uzembe pia waliomba watendaji wa manispaa hiyo wajipime kwani mara nyingi kila wanapomwaga vifusi vya mchanga wamekuwa wagumu kuvisambaza hali inayosababisha wakati mwingine ajali zisizokuwa za lazima kutokea



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post