Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA 15- JINSI SIMBA ALIVYOCHINJWA HADHARANI CCM KAMBARAGE MJINI SHINYANGA

Mashabiki wa Stand na Simba wakichapana makonde uwanjani baada ya shabiki wa Simba(Aliyevaa nguo nyekundu kulia) kukatisha katika jukwaa la mashabiki wa Stand jioni ya leo katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.Katika mchezo huo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa pili Stand United ya Shinyanga imecharaza Simba SC bao 1 kwa 0-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga
 
 Awali mshabiki wa Simba akiwa katika jukwaa la Stand kisha kushushiwa kichapo na mashabiki wa Stand-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Shabiki wa Stand anayejulikana kwa jina la Mwita baada ya kushushiwa makonde na shabiki wa Simba aliyekatisha kwenye jukwaa la Stand United kisha kuanza kushambuliwa
-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga


Ngumi zinaendelea-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Mashabiki wa Stand wakichoma bendera ya Simba iliyokuwa imebebwa na shabiki wa Simba aliyeambulia kichapo uwanjani-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Mashabiki wa Stand United wakichoma bendera ya Simba
-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Wanaendelea kuchoma bendera ya Simba-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Mashabiki wakichoma bendera
-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga


Kocha mkuu wa Simba Golan Kuponovic akikuna kichwa baada ya kupigwa bao 1-0 ambapoa baada ya mchezo amesema Stand siyo timu ya kubeza ni timu nzuri ndiyo maana wameshinda katika mchezo huo-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Awali mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiwasili katika uwanja wa Kambarage kushuhudia mchezo kati ya Stand na Simba ambapo Vijana wake Stand wameibuka washindi katika mchezo huo kwa kuichinja Simba bao 1 kwa nunge
-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Mashabiki wa Stand wakishangilia bao lao
-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Mchezaji wa Stand Abasirim  Chidiebele aliyefunga  bao kwa kichwa katika kipindi cha kwanza akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Wakazi wa Shinyanga wakatumia fursa ya mchezo huo kuokota makopo-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Baada ya mchezo mtaani kukawa hakukamatiki,mashabiki wa Stand wakifanya yao
-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Nguo zikavuliwa kushangilia ushindi wao-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com