Ikiwa ni wiki 2 tu zimepita baada ya bibi aliyedhaniwa kuwa mchawi (80) kukutwa nje ya nyumba ya mtu akiwa uchi hajitambui katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembeza mjini
Shinyanga,matukio yanayohusishwa na imani za kishirikina yameendelea kuacha watu midomo wazi ambapo leo asubuhi binti anayekadiriwa
kuwa na umri wa miaka 23- 25 aliyedaiwa kuwa mchawi amekutwa hajitambui akiwa amevaa nguo nyeusi,kashikilia chungu kidogo kwenye mlango wa nyumba
ya mtu katika mtaa wa Bushushu kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga huku akidai kuwa amefika mahali hapo kwa kutumia chungu-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio nje ya nyumba aliponasa binti huyo anayedhaniwa kuwa mchawi kutokana na nguo alizovaa na dawa nyeusi alizopaka kwenye mwili wake.Binti
huyo kwamba alifika mahali hapo na
wenzake
kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya
Massawe aliyegoma kuoa ndugu yao na badala yake akaoa mwanamke mwingine.
Tukio hili limetokea leo asubuhi katika mtaa wa Bushushu nyumbani kwa Robinson Massawe ambapo binti huyo
alikutwa amelala mbele ya mlango wa nyumba hiyo akiwa hajitambui na baada ya
kusemeshwa ndipo akasimulia yaliyomkuta kwamba alifika mahali hapo na wenzake
zaidi ya 10 kutoka kanda ya ziwa kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya Massawe ili ndugu yao aolewe na baba wa familia hiyo.Kwa mujibu wa ndugu wa baba mwenye nyumba wameiambia Malunde1 blog kuwa kweli ndoa hiyo ilivunjika tangu tarehe 17.9.2014
Pichani binti aliyejitambulisha kwa jina la Coletha akiwa amevaa kishirikina huku mwili wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi akidai
kuwa alikuwa anaongoza wenzake zaidi ya 10 Geita,Mwanza na Shinyanga kuwanga katika
nyumba hiyo.Baada ya kukutwa hapo mlangoni wakazi wa eneo hilo walifika eneo la tukio kisha mwenyekiti wa mtaa huo Ruben Masanja akimwomba mwenye nyumba amruhusu binti aingie ndani kwa usalama wake
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakimhoji binti huyo
ambapo baada ya kumhoji binti huyo
alisema alifika kwenye familia hiyo,akiwa kiongozi wa kundi la wachawi zaidi ya
10 kutoka Ushirombo,Misungwi na Shinyanga wakitumia vyungu na ungo majira ya saa 9 usiku kwa ajili ya kufanya
sherehe baada ya kufanikiwa kusambaratisha kichawi ndoa ya Massawe na Mary
Joseph.
Wananchi wa Shinyanga wakichungulia kilichokuwa kinajiri ndani Askari polisi wakimlinda Binti huyo asipigwe na wananchi waliofika eneo la tukio Wananchi wakisubiri mchawi atoke ndani ya nyumba Askari polisi akimtoa ndani ya nyumba binti huyo ili kumpandisha kwenye gari la polisi Binti akiondolewa eneo la tukio Binti akiwa ndani ya gari la polisi Gari la polisi likiondoka eneo la tukio Wakazi wa Shinyanga wakiondoka eneo la tukio-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI |
Social Plugin