Mez
B alifariki Ijumaa ya February 21 2015 nyumbani kwao Dodoma baada ya
kulazwa hospitali Dodoma zaidi ya mara nne toka mwishoni mwa mwaka 2014,
tatizo kubwa lilikua ni kifua na mgongo ambapo Jumatatu ya February 23
2015 ambapo Mamia
ya mashabiki na wasanii wa muziki wa kizazi kipya,walijitokeza
kuupumzisha mwili wa msanii, Moses Bushangama ‘Mez B’, katika makaburi
ya Wahanga wa Treni, Maili mbili mkoani Dodoma.
Mpaka anafariki Mez B hakuwa ameoa wala hana mtoto ambapo pia
amefariki siku chache kabla ya kuachia single yake mpya kwenye Radio na
TV
Akizungumza wakati wa kuuaga mwili huo, mama wa marehemu, Mchungaji Mary Katambi, aliwataka vijana kumrudia Mungu.
“Mwanangu
aliuona uwepo wa Mungu, nilikuwa nikimsihi kuokoka na kumrudia Mungu na
alikuwa akinijibu itafika wakati mimi wa yeye kufanya hivyo,” alisema Mary.
Upande
wake msanii wa kundi la Chemba Squad, Noorah alisema wamesikitika
kumpoteza Mez B kwani alikuwa ni msanii anayependa ushirikiano na pengo
lake halitaweza kuzibika.
Wananchi
wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Marehemu Mez B baada ya kuagwa na
mashabiki wa mziki pamoja na ndugu jamaa na marafiki mwili wake
ulielekea kupumzishwa katika makaburi ya Wahanga Maili mbili jana.
Mama
mzazi wa Mez B, Marry Mkandawile (katikati) akiwa ameshikiliwa na ndugu
baada ya kuingia viwanja vya Mashujaa ili kutoa heshima za mwisho.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria msiba wa Mez B wakiwa kwenye majonzi mazito
Mtangazi wa Citizen TV anayejulikana kwa jina la Mzazi Willy Tuva akifanya mahojiano na msanii wa Bongo Fleva Janjaro.
~mpekuzihuru
Baadhi ya Wasanii waliojitokeza kumzika ni pamoja na Dogo Janja na Raymond wa Tiptop Connection, Hemedy PHD, Gelly wa Rymes, Baba Levo, M2theP, Noorah na Dark Master kutoka Chemba Squad.