Awali mkurugenzi wa Shule ya Kom sekondari Jackton Koyi akimkaribisha Patrick Kluivert katika shule yake kwa ajili ya kufungua jengo la michezo katika shule hiyo |
Kushoto ni mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akizungumza katika shule ya Sekondari KOM ambapo
alisema lengo la kufungua kituo hicho ni kuinuna vipaji vya watoto wenye
uwezo wa kucheza mpira kwani siku zote kipaji huonekana kwa mtu akiwa bado
mdogo.
Masele alisema Jengo hilo litakuwa na vifaa vyote vya michezo ikiwemo Gym na
kuwatakia kila la heri wale wote watakaopata nafasi ya kutumia kituo hicho.Wa kwanza kulia ni Patrick Kluivert
Patrick Kluivert akizungumza jambo na mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele
Muda mfupi baada ya kuwasili katika shule ya Kom Sekondari,mheshimiwa Stephen Masele(wa tatu kutoka kushoto) akiwa na mgeni wake Patrick Kluivert( wa pili kushoto),mkurugenzi Kom Sekondari Jackton Koyi( wa kwanza kushoto) na mwalimu wa michezo KOM Sekondari Michel Odelo( wa kwanza kulia) wakielekea kwenye jengo la michezo katika shule hiyo jana jioni
Mwalimu KOM Sekondari akiongoza msafara kuelekea kwenye jengo la Michezo kwa ajili ya ufunguzi wa kituo cha Michezo katika shule hiyo
Mkurugenzi wa KOM Sekondari Jackton Koyi akitoa maelekezo kwa wageni wake
Msafara kuelekea kwenye jengo la michezo katika shule ya sekondari Kom kwa ajili ya ufunguzi Baada ya kufungua kituo hicho cha michezo,hapa ni mbele ya jengo hilo Mheshimiwa Masele akipiga makofi na wadau wengine wa michezo |
Baada ya ufunguzi Patrick
Picha ya pamoja Patrick Kluivert na walimu wa Kom Sekondari,wa pili kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku,wa kwanza kulia ni
Mwalimu wa michezo KOM Sekondari Michel Odelo alisema wamefurahishwa na
ujio wa Kluert na kwamba ujio wake utakuwa chachu ya kuinua vipaji vya
wachezaji wa mpira na kuwaomba wazazi kupeleka wenye vipaji vya kucheza mpira
katika kituo hicho ili kutengeneza wachezaji wazuri wa baadaye watakaousaidia
mkoa wa Shinyanga na Taifa kwa ujumla katika michezo.
|
Wakuu wa wilaya za Shinyanga na Kishapu nao walikuwepo,wa kwanza kushoto ni Wilson Nkhambaku wa Kishapu akifuatiwa na Annarose Nyamubi wa Shinyanga |
Picha za kumbukumbu zikaendelea kupigwa hapo Kom sekondari |
Patrick Kluivert na Wanamichezo wa KOM Sekondari |
Mkurugenzi wa KOM Sekondari Jackton Koyi akiwa na Patrick Kluivert-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga BOFYA HAPA UONE PATRICK KLUIVERT ALIPOKUTANA NA STAND UNITED UWANJA WA KAMBARAGE SHINYANGA |
Social Plugin