Hatimaye kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti la Ijumaa kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiitaKaisi Bin Abdullah(PICHANI) akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!
Gazeti
hilo linadai kuunasa mkanda huo kutoka kwa mtu mmoja aliyekataa
kujitambulisha kwa jina wala kusema anakotokea hapa nchini.
Bin Abdullah ametumia dakika 11: 03 kuzungumzia mambo mbalimbali lakini kubwa kuliko yote ni kuliponda Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuwakamata wenzao katika imani na harakati (zinazohifadhiwa kwa sasa) na kuwashikilia kwenye mahabusu mbalimbali nchini.

Alianza kwa Kusema:
Bin
Abullah ambaye kwenye mkanda huo amevaa nguo nyeusi kama ninja na
miwani ya giza, alizungumza kwa kirefu, akitoa wito lakini mbele
akasema:
“Tumeshaungana
ili kupambana. Mkoa wa Mtwara zaidi ya wenzetu kumi na saba walikamatwa
kwa makosa ya dhuluma, makosa ya kupanga, makosa ya ugaidi.
Ishirini na moja wamekamatwa Zanzibar wako katika Gereza la Segerea (Dar). Wenzetu wengine kumi na nane wamekamatwa Mwanza wako katika Gereza la Kisongo, Arusha. Ndugu zangu, wenzetu wengine kumi na saba wameuawa Mtwara kwa amri ya ...(anamtaja waziri).”

“Subira
yetu imefika mwisho na tulichokuwa tunasubiri Mungu ameshatupa. Tunatoa
ahadi kilichopo hivi sasa tunatoboa jahazi wote tuzame.
“Tunatoa rai, wenzetu waliopo Gereza la Kisongo waachiwe huru. Hapa hatumtishi mtu yeyote yule.”
“Pili,
agizo la Ernest Mangu IGP, umetangaza uliwenguni kwamba umewakamata
wote waliovamia vituo vya polisi na umezikamata silaha zote. Ukweli ni
kwamba unatetea tumbo lako. Hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa na wala
silaha hazijakamatwa.
“Mungu
ametukubali. Katika Kituo cha Polisi Ushirombo (Kilimanjaro) tumeweza
kuvamia kituo, tukaweza kutoa roho za polisi na tukaweza kuchukua
silaha, tunazo.
“Tumevamia Kituo cha Polisi Ikwiriri (Pwani), tumeweza kuchukua silaha za kutosha, tumeweza kuchukua mabomu ya kutosha. Tunazo silaha tunasubiri muda zianze kufanya kazi.
“Tumevamia Kituo cha Polisi Ikwiriri (Pwani), tumeweza kuchukua silaha za kutosha, tumeweza kuchukua mabomu ya kutosha. Tunazo silaha tunasubiri muda zianze kufanya kazi.
“Ernest Mangu nakupa changamogto, hivi sasa tuna uwezo...(maneno yanahifadhiwa kwa usalama) wakati wowote ambao tunataka.
“Tumeweza
kuchukua silaha bila kuwa na silaha yoyote. Ndugu zetu wa Tanga
wameweza kuchukua silaha wakiwa hawana silaha yoyote. Ikwiriri
tumechukua silaha tukiwa hatuna silaha yoyote, mpaka sasa tumeshachukua
roho tano za polisi.
“Ndugu zangu, ...mlikuwa mkinisubiri nitoe tamko, natoa kauli rasmi...”alihitimisha
Abdullah, huku vitisho vya jumla kwenye tamko lake vikiwahusu polisi,
viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na mikusanyiko ya ibada.
Tamko la IGP
Baada
ya video hiyo,Gazeti la Ijumaa lilimtafuta Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania, IGP Ernest Mangu na kuzungumza naye kuhusu mtu huyo na
kumkabidhi video ambapo alisema:
“Nawashukuru
sana kwa kuleta video hii, huu ndiyo ushirikiano unaotakiwa, nawaomba
wananchi video za aina hii wazikatae kwa sababu ni kosa kuwa nazo na
watu kadhaa wameshakamatwa kwa kuwa nazo.
“Sisi
kama jeshi la polisi tunajua kuwa kuna watu wanadhani kufanya uhalifu
kama huo kutawasaidia kutimiza matakwa yao, lakini ukweli ni kwamba
polisi wapo imara na nina uhakika watuhumiwa watakamatwa kwa
kushirikiana na raia wema.”
Shehe Mkuu Amkana
Baada
ya kuzungumza na IGP, Gazeti lilimtafuta Shehe Mkuu Tanzania, Mufti
Shaban Simba na kumsimulia kuhusu kuibuka kwa Bin Abullah na kutaka
kujua pengine anamfahamu.
“Kwanza
hizo taarifa hizo ndiyo nazisikia kutoka kwako. Hilo jina ulilonitajia
(Bin Abdullah) sijawahi kulisikia labda muangalie kwa wenzetu upande wa
pili.”
Chanzo: Gazeti la Ijumaa/Gpl
Chanzo: Gazeti la Ijumaa/Gpl
Social Plugin