Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MKUTANO WA MWAKA WA RCC MJINI DODOMA


Hapa ni katika ukumbi wa New Dodoma Hotel mjini Dodoma ambapo leo umeanza mkutano wa siku tatu wa kwanza wa mwaka wa kamati za mikoa za baraza la ushauri la watumiaji wa huduma zinazothibitiwa na Ewura( RCC Annual Conference) lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya namna kuongeza ufanisi katika kutekelezaji wa majukumu yao na kukumbushana juu ya malengo ya Baraza na dhana nzima ya udhibiti na utetezi wa masilahi ya mtumiaji wa huduma za nishati na maji-picha zote na Kadama Malunde na Stella Lupimo- Dodoma
 

Awali  Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na Ewura Eng Profesa Jamidu Katima akifungua mkutano huo ambapo alisema watanzania wengi hawapati taarifa na maelezo sahihi kuhusu masuala ya udhibiti sambamba na ongezeko la malalamiko ya watumiaji wa huduma zinazdhibitiwa na EWURA na kuongeza kuwa baraza linajukumu kubwa kuhakikisha kuwa watumiaji wa huduma za maji na nishati wanapata taarifa sahihi na kwa wakati ikiwa ni pamoja na utoaji elimu ya haki na wajibu wa watumiaji.


Prof Katima alisema katika kufanikisha azma ya kufikisha elimu kwa watumiaji baraza limeandaa mkakati na sera ya mawasiliano 2014/2018 ambao umeanza kutekelezwa tangu mwaka 2014.



Mkutano huu umezikutanisha kamati zote za watumiaji wa huduma za nishati ya maji kutoka mikoa 24 ya Tanzania bara,ambapo mkutano huo utatoa fursa ya kamati hizo kujitathmini juu ya mafanikio yaliyofikiwa toka kuanzishwa kwake,changamoto zinazoikumba kamati katika utekelezaji wa majukumu yake na kuweka mikakati ya kutatua changamoto hizo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Picha za pamoja wakati wa mapumziko leo asubuhi katika makundi mbalimbali

Picha za pamoja

 Picha ya pamoja
zoezi la kupiga picha za pamoja linaendelea

Mkutano unaendelea

Mkutano unaendelea-picha zote na Kadama Malunde na Stella Lupimo- Dodoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com