Moja ya taarifa kutoka Nairobi Kenya
ambayo ilisikitisha sana ni tukio la watoto watatu kuuawa na mwanamke
mmoja ambaye baada ya kuwaua halafu akawapasua na kula mioyo ya watoto
hao.
Mwanamke huyo Catherine Muthoni alimuua mtoto wake mmoja mwenye umri wa miaka kumi na baadaye kuua watoto hao wawili wa jirani.
Tukio la leo katika eneo la makaburi ya
Lang’ata limewatoa wengi machozi wakikumbuka jinsi watoto hao
walivyofariki kwa mateso ambapo familia ya watoto hao wameamua kufanya
mazishi ya watoto wote wawili kwenye kaburi moja.
Mwanamke huyo anashikiliwa na Polisi
kesi yake ikiendelea ambapo Mahakama iliagiza afanyiwe uchunguzi kama
ana matatizo ya akili huku upelelezi wa kesi yake ukiendelea.
Hii Hapa taarifa hiyo kwenye video kutoka K24 TV Kenya
Hii Hapa taarifa hiyo kwenye video kutoka K24 TV Kenya
Social Plugin