Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MCHEZAJI GWIJI NA NYOTA PATRICK KLUIVERT APOKELEWA KWA KISHINDO SHINYANGA, AKUTANA NA STAND UNITED


Mji wa Shinyanga jioni ya leo umetekwa na kocha namba 2 wa timu ya taifa ya Uholanzi wakati wa kombe la dunia na mchezaji gwiji na nyota wa zamani wa Ajax Amstadam, Barcelona ya Hispania na NewCastle ya Uingereza Patrick Kluivert bingwa wa mipira ya vichwa aliyekuwa ameambatana na na gwiji wa zamani wa Barcelona na Real Madrid Rayco Garcia ambaye ni Scout wa Real Madrid,ambao wamekutana na Wachezaji wa Timu ya Stand United FC maarufu Chama la Wana  pamoja na mashabiki wa soka kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga kuwapa mbinu mbalimbali za kufanikiwa kisoka-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Wachezaji wa Stand United wakiwasili Uwanjani


Kushoto ni Patrick Kluivert akipokelewa uwanjani-Tukio zima lilikuwa katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga chini ya udhamini wa mbunge wa Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Rais anayesimamia Muungano na Mazingira lengo likiwa ni kusaka vipaji vya soka kwa ajili ya kucheza ligi za ulaya,kukuza michezo na kuitangaza Shinyanga nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania.

Patrick Kluivert  akisalimiana na wapenzi wa soka mkoa wa Shinyanga wakati akipanda jukwaa kuu

Jukwaa Kuu-Aliyevaa Miwani ni mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele aliyemleta Patrick Kluivert(kulia kwake),wa kwanza kulia mbele ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Annarose Nyamubi

Kulia ni Patrick Kluivert akifuatilia mazoezi yaliyokuwa yanafanya na wachezaji wa Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage kabla ya kuongea nao na kuwapa siri ya mafanikio katika soka ili waweze kucheza ligi za ulaya

Mbunge wa Shinyanga Stephen Maselea akiongea jambo baada ya kushuka kutoka jukwaa kuu na kuingia uwanjani ili Patrick Kluivert azungumze na wachezaji wa Stand United
Wa kwanza kushoto ni Mwandishi wa habari gazeti la Nipashe na Malunde1 blog Marco Maduhu akiwa uwanjani
Patrick Kluivert akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Stand United wakati wa zoezi maalum jioni ya leo lengo ni kuwanoa ili wawe tishio ndani na nje ya Tanzania

Wa kwanza kushoto ni afisa Habari wa Stand United Isaack Edward akifuatiwa na mkurugenzi wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde wakiwa na Patrick Kluivert wakifuatilia zoezi maalum la wachezaji wa Stand united
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Khambaku akibadilishana  mawazo na nyota wa zamani wa Timu ya taifa ya Uholanzi na Barcelona Patrick Kluivert katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga
Mbunge wa Shinyanga mjini  Stephen akimtambulisha Patrick Kluivert kwa wachezaji wa Stand United

Patrick Kluivert  akizungumza na wachezaji wa Stand United
Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku,aliyekuja kushuhudia zoezi hilo maalum la Stand FC akiwa na Patrick Kluivert leo uwanjani
Picha ya pamoja wachezaji wa Stand United na Patrick Kluivert
 Patrick Kluivert akifanya yake uwanjani
 Picha ya pamoja na wachezaji wa Stand United
Picha ya pamoja na Patrick Kluivert

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza uwanjani hapo ambapo mbali na kumpongeza mbunge wa Shinyanga Mjini kwa kazi nzuri katika kuisadia Stand United pia aliwataka wachezaji wa Tmu hiyo kutumia fursa ya kocha namba 2 wa timu ya taifa ya Uholanzi wakati wa kombe la dunia na mchezaji gwiji na nyota wa zamani wa Ajax Amstadam, Barcelona ya Hispania na NewCastle ya Uingereza Patrick Kluivert bingwa wa mipira ya vichwa kufanya mambo makubwa

Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akimkaribisha gwiji wa zamani wa Barcelona na Real Madrid Rayco Garcia ambaye ni Scout wa Real Madrid ili azungumze na mashabiki wa soka mkoani Shinyanga

 Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akimkaribisha
Patrick Kluivert ili azungumze na wakazi wa Shinyanga


Wakazi wa Shinyanga wakiwa wamekaa mkao wa kula kumsikiliza Patrick Kluivert
Patrick Kluivert akizungumza na wakazi wa Shinyanga,ambapo pia mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku alikuwepo( wa pili kutoka kushoto)

Patrick Kluivert akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema anataka kuisaidia timu ya Stand United ili iweze kupeleka wachezaji wake kucheza mechi za nje ya nchi

Wapenzi wa soka wanafuatilia kilichokuwa kinaendela uwanjani

Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendela uwanjani-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
BOFYA HAPA UONE PATRICK KLUIVERT AKIFUNGUA KITUO CHA MICHEZO KOM SEKONDARI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com