Unakumbuka ile Stori ya askari Asuma Mpaji na Veronica Nazaremo
kufukuzwa kazi Mkoani Kagera baada ya picha zao kusambaa mitandaoni
wakionekana kupigana mabusu? safari hii nakuletea tena stori inayofanana
na hiyo ambayo imetokea Nchini Uingereza.
Polisi wa nchi hiyo ya
Uingereza waliamua kumshtaki mwenzao baada ya kufanya kitendo cha
kudhalilisha jeshi la nchi la nchi hiyo kwa kufanya tendo la ndoa tena
mbele za watu akiwa na sare za kazi.
Kitendo hicho kimemfanya kufukuzwa kazi
bila kupewa taarifa za awali haraka baada ya kwenda kwenye shughuli zake
za kila siku za usalama na kufanya kitendo hicho huku akijua ni kinyume
na sheria tena akiwa amezungukwa na watu.
Msaidizi mkuu wa kituo hicho Russ Middleton alisema wanaamini hatua hiyo itakua fundisho kwa wengine kutokana na kitendo hicho cha udhalilisha.
Kwa upande mwingine polisi mwingine nchini Uruguay naye alikumbwa na mkasa unaofanana na huo baada ya kucheza na mwanamke akiwa uchi katika kituo chake cha kazi.
Picha ya askari huyo zilinaswa na
mitandano mbalimbali na kujikuta zikisambaa kwa kasi hali iliyosababisha
ashtakiwe kwa kosa hilo.
Social Plugin