Mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo
dereva msaidizi wa basi aliyejitambulisha kwa jina moja la Makubeli
akisema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya basi kuharibika mfumo wa breki
na kumshinda dereva mwenzake kauli inayopingana na mmoja kati ya abiria
aliyekuwemo kwenye basi hilo ambaye anadai chanzo ni mwendo kasi ambapo
dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita basi jingine lililokuwa mbele
yao bila tahadhari na ghafla akakutana uso kwa uso na lori.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Sasp David Misime amesema chanzo
cha ajali kimetokana na dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T 663
AXL aina ya Scania alipokuwa akijaribu kulipita gari lingine bila
kuchukua tahadhari na kukutana uso kwa uso na lori lenye namba za
usajili T 496 CFG likiwa na tela namba T 576 AXZ ambapo watu wawili
waliofahamika kwa majina ya Fadhili Saidi dereva wa lori na Chogo
Chigunda utingo wa basi wakafariki dunia.
Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Dodoma Dk
Nasoro Mzee amethibitisha kupokea maiti hizo mbili na majeruhi 44 ambapo
16 wametibiwa na kuruhusiwa huku wengine 27 wakilazwa.