Bi
harusi mmoja kaskazini mwa India, amejikuta kwenye wakati mgumu siku ya
ndoa, kisa ni ugonjwa wa mume wake mtarajiwa ambao yeye hakujua kama
bwana huyo anaumwa.
Haikuwa siku nzuri kwa bwana harusi, ana tatizo la ugonjwa wa kifafa na tatizo hilo likamkuta siku ya ndoa yake na bibie Indra.
Indra alifanya maamuzi hayo magumu ambapo muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na bwana Jugal Kishore, bwana
huyo alianguka ghafla kutokana na kifafa na kupelekwa Hospitali kwa
ajili ya kupatiwa matibabu, tukio hilo lilimfanya Bi harusi ashikwe na
hasira kutokana na mume wake huyo mtarajiwa kumficha kwamba ana tatizo
la ugonjwa huo.
Indra alibadili
maamuzi, akatoa ombi la kuolewa na mmoja wa wanafamilia ya bwana
harusi, ambaye alikuja tu harusini kusherehekea sherehe hiyo, jamaa
akaona hii ni bahati ya mtende kwake, baada ya bwana harusi kupata
nafuu alirudi na kukuta story imekuwa nyingine harusini.
Hii mfano inakutokea wewe ungeamua nini mtu wangu?
Social Plugin