Pichani ni binti huyo akiwa ameuawa na watu wasiojulikana |
Mwanamke mmoja
aliyefahamika kwa jina la Huma Simon (27) mkazi wa kitongoji cha Solwa
Kata ya Solwa Wilayani Shinyanga Vijijini ameuawa kwa kukatwa mapanga na
watu wasiojulikana usiku wa kuamkia siku ya Alhamis Februari 19,2015.
Kwa mujibu wa Majirani
Mwili wa marehemu Huma umekutwa asubuhi katika eneo la Shule ya msingi
Solwa ukiwa umekatwa mapanga sehemu mbalimbali na kutelekezwa.
Taarifa zimesema Huma
ambaye anaishi na Mama yake Mzazi, alitoka usiku katika chumba alichokuwa
amelala na kumuacha Mtoto wake wa kike anayekadiriwa kuwa na miaka
miwili, na kukutwa asubuhi akiwa ameuawa.
Social Plugin