Siku chache tu baada ya bibi aliyedhaniwa kuwa mchawi mwenye
umri wa miaka 80 kukutwa nje ya nyumba ya mtu akiwa uchi huku Ndembeza mjini
Shinyanga leo binti anayekadiriwa
kuwa na umri wa miaka 23- 25 anayedaiwa kuwa ni mchawi amekutwa kwenye mlango wa nyumba
ya mkazi wa mtaa wa Bushushu kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga
akiwa amejifunga nguo nyeusi huku mwili wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi usoni,mikononi,mgongoni na miguuni,alidai
alikuwa anaongoza wenzake zaidi ya 10 kutoka Geita,Mwanza na Shinyanga waliofika kuwanga katika
nyumba hiyo.
Binti huyo amekutwa leo asubuhi nyumbani kwa Robinson Massawe ambapo binti huyo alikutwa amelala mbele ya mlango wa nyumba hiyo akiwa hajitambui na baada ya kusemeshwa ndipo akasimulia yaliyomkuta kwamba alifika mahali hapo na wenzake kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya Massawe aliyegoma kuoa ndugu yao na badala yake akaoa mwanamke mwingine.
|
Social Plugin