BONDIA FRANCIS CHEKA AHUKUMIWA JELA MIAKA 3 KWA KUMPIGA NGUMI MTU


 Bondia maarufu nchini Fransic Cheka baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 3 leo mchana baada ya kumpiga mangumi meneja wake ....

Picha za Kwanza za Bondia Maarufu Akipanda Gari Kuelekea Kuanza Kifungo Chake Leo

Taarifa iliyoifikia Malunde1 blog hivi punde,inaeleza kuwa Bondia maarufu hapa nchini,Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha Miaka mitatu (3) jela kwa kukutwa na hatia ya kumpiga na kumjeruhi Meneja wa  Bar yake iliyopo mjini Morogoro.
Cheka alifikishwa kizimbani leo na kusomewa mashtaka ya kushambulia na kuzuru mwili,akidaiwa mnamo julai 02 mwaka 2014, bila uhalali na akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria, alimpiga kwa ngumi maeneo ya kichwani na tumboni, Bahati Kabanda maarufu kama Masika, na kumsababishia maumivu makali.

Hukumu hiyo imetolewa leo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi,Mkoani Morogoro.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post