Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE KAPTENI JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA


Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni.

Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.

"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa nyumbani amekaa lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye kidogo alifariki" amesema Jerry Komba mtoto wa marehemu.


Mmoja wa madaktari aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni leo akiwa mahututi .


"Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia," amesema Dk Ishan

Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo cha mareheme, hata hivyo amesea Kapteni Komba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.


Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.

Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.




ANGALIA PICHA MAREHEMU KOMBA ENZI ZA UHAI WAKE KATIKA MATUKIO TOFAUTI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com