Moja ya taarifa ya kushtua na
kuhuzunisha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na watu
kutumiana message ni kuhusu msiba wa aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo
Fleva, katika kipindi cha LEO TENA wametafutwa watu wa karibu ili
kuthibitisha taarifa hiyo.
Dada wa marehemu ambaye jina lake ni Rachel amethibitisha kuwa msanii MEZ B amefariki akiwa nyumbani kwao Dodoma.
Noorah ni msanii ambaye walikuwa karibu na Mez B,
amesema Mez B alikuwa na homa tangu mwezi December mwaka jana na
baadaye akasafiri kwenda Dodoma huku hali yake ikiwa bado sio nzuri,
mara ya mwisho wameongea kwenye simu ni siku tano zilizopita, leo simu
yake imepokelewa na dada yake akimtaarfu kuwa Mez B amefariki muda mfupi uliopita baada ya kuzidiwa.
Mez B aliwahi kuwa kundi moja Chamber Squad na akina Ray C, Noorah na marehemu Albert Mangwea pia.
Msiba uko nyumbani kwao eneo la Kisasa, Dodoma.
millardayo.com itakusogezea taarifa zaidi kutoka msibani Dodoma kila zinaponifikia, #RIP Mez B.
Hii sauti kutoka kwenye Leo Tena @CloudsFM, kasikika NOORAH, TIMBULO na RACHEL ambaye ni dada wa MEZ B.
Social Plugin