Waziri mkuu Mizengo Pinda akilia kutokana na mauaji ya albino chini Tanzania-Picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog |
Mwili wa mtoto Yohana Bahati
aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi maarufu kama
Albino, alitekwa siku ya Jumapili February 15, 2015 amepatikana ameuawa
katika eneo la Shilabela Mapinduzi kilomita kadhaa kutoka nyumbani kwao
kijiji cha Ilelema .
Polisi wanaeleza kuwa waliukuta mwili huo katika
msitu wa hifadhi wa Biharamulo leo majira ya alfajiri akiwa amekatwa
mikono na miguu yake.
Madaktari walimfanyia upasuaji mwanamke huyo aliyekuwa amekatwa kwa panga usoni mwake na sehemu zingine za mwili majeraha ambayo aliyapata wakati alipokuwa akijaribu kumuokoa mwanawe, Yohana kutoka mikononi mwa wauaji .
Dada zake Yohana Tabu bahati mwenye umri wa miaka mitatu bado yuko mikononi mwa uangalizi wa askari polisi.
Dada yao mkubwa ambaye pia ni Albino Shida Bahati mwenye umri wa miaka kumi na miwili amehamishwa kijijini hapo tangu tukio hilo litokee, na anatunzwa na jamaa zake katika kijiji jirani.
Mpaka sasa watu wengine wawili zaidi wamekamatwa na polisi wakihusishwa na tukio hilo ingawa baba mzazi wa mtoto huyo, bado anashikiliwa na polisi.
Mwezi uliopita serikali ya Tanzania ilipiga marufuku waganga wa kienyeji pia kupiga marufuku wapiga ramli wote ambao wanaelezwa kuchangia mauaji ya watu hao wenye ulemavu wa ngozi.. waganga wa kienyeji wanaamini kwamba viungo vya mwili wa Albino huleta bahati na utajiri kwa anaye vipata.katazo hilo ni sehemu ya mkakati maalumu wa kupunguza
kama sio kuondosha kabisa mashambulizi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Social Plugin