Duh!! JAMAA AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMNYONGA WAKIFANYA MAPENZI GESTI USIKU


Kijana mmoja mkazi wa Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam amemua   mwanamke kikatili kwa kumnyonga hadi kufa katika nyumba ya kulala wageni ya Stav iliyopo eneo la Kichangani mjini Morogoro.

Kamanda poilsi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema jeshi la polisi linamshikilia kijana atwaye Erick Bruno (30) mkazi wa Manzese baada  kumuua  mwanamke aitwaye Jada Dungu mkazi wa Kichangani mjini Morogoro kwa kumnyonga hadi kufa usiku wakati wakiwa wamelala katika nyumba ya wageni na mtuhumiwa anahojiwa na atafikishwa mahakamani.
Nao wananchi walioshuhudia tukuio hilo wamesema usiku walisikia marehemu akipiga kelele akiomba msaada ambapo walienda katika tukio katika nyumba ya kulala wageni ndipo wakavunja mlango na kufanikiwa kumkakata mtuhumiwa akijiandaa kutoroka baada ya kufanya mauaji.
Katika tukio jingine mtu mmoja amekutwa amekufa katika boma la waliloishi watu huku mwili wake ukiwa umeharibika katika eneo la Mji mpya katika manispaa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema mtu huyo alifahamika kwa majina ya Anton Mbulu na mwili wake umechuKuliwa na jeshi la polisi na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post