Kijana
mmoja mkazi wa Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam amemua mwanamke
kikatili kwa kumnyonga hadi kufa katika nyumba ya kulala wageni ya Stav
iliyopo eneo la Kichangani mjini Morogoro.
Kamanda poilsi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema jeshi la polisi
linamshikilia kijana atwaye Erick Bruno (30) mkazi wa Manzese baada
kumuua mwanamke aitwaye Jada Dungu mkazi wa Kichangani mjini Morogoro
kwa kumnyonga hadi kufa usiku wakati wakiwa wamelala katika nyumba ya
wageni na mtuhumiwa anahojiwa na atafikishwa mahakamani.
Nao wananchi walioshuhudia tukuio hilo wamesema usiku walisikia
marehemu akipiga kelele akiomba msaada ambapo walienda katika tukio
katika nyumba ya kulala wageni ndipo wakavunja mlango na kufanikiwa
kumkakata mtuhumiwa akijiandaa kutoroka baada ya kufanya mauaji.
Katika tukio jingine mtu mmoja amekutwa amekufa katika boma la waliloishi watu huku mwili wake ukiwa umeharibika katika eneo la Mji
mpya katika manispaa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia
tukio hilo wamesema mtu huyo alifahamika kwa majina ya Anton Mbulu na
mwili wake umechuKuliwa na jeshi la polisi na uchunguzi wa tukio hilo
unaendelea.
Social Plugin