Mratibu wa mradi wa EGPAF mkoa wa Mtwara na Lindi Dr Joseph Obedi akitoa maelezo ya kazi za EGPAF mkoani Lindi kwa kaimu mkurugenzi mtendaji wa mkoa wa Lindi John Likango |
Mratibu
wa mawasiliano na Utetezi wa EGPAF bi Mercy Nyanda akizungumza na mama
Matilda Barnaba, Mkazi wa Lindi mjini ambaye alifanikiwa kuchunguzwa na
kufanyiwa matibabu ya dalilili za awali za saratani
ya mlango wa kizazi katika hospitali ya Sokoine, Lindi mwezi Desemba,
2014.
Mhudumu wa Afya, bi Monica Ikoni wa hospitali ya Wilaya ya Nachingwe
akitoa maelezo ya jinsi ya kufanya tiba ya awali kwa wamama
waliogundulika na dalili za mwanzo za saratani ya mlango wa kizazi .
Monica ni mmoja wa wahudumu wa
afya waliopatiwa mafunzo hayo na EGPAF
Mratibu wa kituo cha matibabu na matunzo kw a watu wanaoishi na VVU , cha hospitali ya mkoa wa Lindi, Dr. Hamis Ajali, akiongea na waandishi wa habari mkoani Lindi. |
Shirika
lisilo la kiserikali la Elizabeth Glaser Pediatric AIDS
Foundation(EGPAF) linalofadhiliwa Serikali ya watu wa Marekani kupitia
mashirika yake ya CDC na USAI D
limewezesha upatikanaji wa huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa
kizazi kwa akina mama mkoani Lindi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani Lindi, Mratibu wa mawasiliano wa Shirika
la EGPAF bi Mercy Nyanda ameeleza kuwa. Shirika hilo limeanza kusaidia
upatikanaji wa
huduma hizo mkoani Lindi mwaka 2012. Na hospitali zilizowezeshwa utoaji
wa huduma hizo ni pamoja na hospitali ya Mkoa ya Sokoine, Hospitali ya
Wilaya ya Nachingwea pamoja na hospitali ya wilaya ya Kilwa- Kinyonga.
Alisema kuanzia
mwezi Januari, 2014 mpaka Desemba 2014 jumla ya akina mama 385 walifanyiwa
uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na miongoni mwao akina mama 26
walibainika kuwa na dalili
za awali za saratani hiyo na akina mama 12 walipewa Rufaa kwenda hospitali
ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Naye
afisa mradi, mafunzo wa EGPAF mkoa wa Mtwara na Lindi, Bw. Ali Kipande
amesema ili kusaidia ufanisi wa huduma hizo, EGPAF kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, imetoa
mafunzo ya uchunguzi wa saratani hiyo na matibabu ya awali kwa watoa
huduma 13 katika mkoa wa Lindi.