HABARI NJEMA KWA WAPENZI WA SOKA MKOA WA SHINYANGA


Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Rais anayesimamia Muungano na Mazingira anawakaribisha wadau na wapenzi wa soka wa Shinyanga kuhudhuria mazoezi maalumu ya timu yetu ya Stand United.

Mazoezi hayo yatakayotolewa na kocha namba 2 wa timu ya taifa ya Uholanzi wakati wa kombe la dunia na mchezaji gwiji na nyota wa zamani wa Ajax Amstadam, Barcelona ya Hispania na NewCastle ya Uingereza Patrick Kluivert bingwa wa mipira ya vichwa yatakayofanyika katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.

 Lengo kuu ni kusaka vipaji vya soka kwa ajili ya kucheza ligi za ulaya.

Kluivert ameambatana na gwiji wa zamani wa Barcelona na Real Madrid Rayco Garcia ambaye ni Scout wa Real Madrid.

Wote ni marafiki wa karibu wa mheshimiwa mbunge  Masele wamekuja kwa lengo la kuitangaza timu ya Stand United kimataifa.

Wote mnakaribishwa kuanzia saa nane mchana siku ya Jumatano tarehe 11/02/2015.

Ziara hii imedhaminiwa na mbunge wa Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele kwa malengo ya kukuza michezo na kuitangaza Shinyanga nje ya mipaka ya nchi(kimataifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post