Hali ya Esther Jonas, ambaye ni mama
mzazi wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyetekwa na kufariki dunia
baada ya kukatwa viungo, imeelezwa na madaktari wa hospitali ya rufaa
Bugando jijini Mwanza alikolazwa kuwa ni mbaya baada ya kushindwa kupumua kutokana na
kuvimba sehemu kubwa ya mwili ikiwamo kichwani.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye jana
alifanyiwa upasuaji wa kichwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando na hali yake
imebadilika ghafla usiku wa kuamkia leo na madaktari wamemuwekea mipira
puani kwa ajili ya kumsaidia kupumua ili kuokoa maisha yake.
Mkuu wa kitengo cha dharura katika hospitali hiyo Dk. Derick
David amesema kuwa hali ya mama huyo sio nzuri na kwamba kwa sasa
anapumua kwa shida na pia hazungumzi na kuongeza kuwa kinachofanyika
sasa ni kuendelea kumsafisha vidonda na kumpa antibaotiki ya kukausha
vidonda.
Mwenyekiti wa chama cha walemavu wa ngozi mkoani mwanza Alfred Kapole ametoa tamko kuhusiana na tukio hilo.
Mwanamke huyo mkazi wa kijiji cha ilelema wilayani chato mkoani Geita alishambuliwa na watu wasiojulikana na kisha kuporwa mtoto wake
mwenye ulemavu wa ngozi – albino aitwaye Yohana Bahati mwenye umri wa
mwaka mmoja aliyekuwa amebebwa mgongoni wakati akipika chakula cha
usiku.
via>>ITV