Hatari!! KIJANA ALIYEKIMBIA ASKARI POLISI AKAMATWA AKIWA NA RISASI 356 ZA SMG/SAR HUKO TABORA

Jumla ya risasi 356  za SMG/SAR zilizokamatwa askari Polisi  kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Wolfram Msemwa(32) huko katika mtaa wa Kazehill kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora.
Risasi hizo
Kitambulisho cha mtuhumiwa aliyekutwa na risasi hizo ambaye kabla ya kukamatwa tarehe 2/2/2015 aliwahi kuwakimbia askari Polisi  mnamo tarehe 23/11/2014 na kutelekeza begi alilokuwa amehifadhi bunduki aina ya SMG na risasi 17 katika eneo la Mazinge hospitali ya wilaya ya Sikonge

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Juma Bwire akiwaonesha waandishi wa habari risasi zilizokamatwa katika operesheni maalumu iliyofanikiwa kumtia nguvuni kijana huyo Wolfram Msemwa anayedaiwa amekuwa na mtandao na baadhi ya waharifu kutoka nchi jirani na Tanzania kwa upande wa Magharibi.

Jeshi la polisi mkoani Tabora limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa matukio ya uharifu huko katika kata ya ngambo manispaa ya Tabora, akiwa na risasi 356 za silaha za SMG/SAR, zilizosadikiwa kuwa, zilikuwa zitumike, katika matukio ya  uharifu katika mikoa ya Tabora, Kigoma ,Mbeya, na Njombe. 

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishima msaidizi Juma Bwire amemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la Warfram Benard Msemwa, mkazi wa Sikonge, ambaye alikuwa akitafutwa na jeshi hilo kutokana na kutelekeza begi lililokuwa na silaha aina ya SMG na risasi 17, huko katika eneo la kituo cha afya cha Mazinge wilayani humo. 
 
Aidha Acp Juma Bwire amesema kuwa, katika kumhoji mtuhumiwa huyo amekiri kuwa na mawasiliano ya kiuharifu na watu furani katika nchi jirani ya Burundi ambapo zinatoka risasi hizo pamoja na siraha, ambayo aliiteklekeza hapo awali kwa kuwahofia polisi aliowaona kwa mbali, na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post