Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia baadhi ya nyumba zimefungwa ambapo wakizungumza
wakiwa maporini wanawake hao wamesema baadhi ya watu wameyakimbia makazi
yao kutokana na kuishi kwa hofu ambapo wamesema migogoro hiyo ya ardhi
inawaathiri wanawake na watoto zaidi kwani wanaume wamekimbia na
kuwaachia mzigo wa kulea familia huku wengine wakikosa msaada na wengine
wakishindwa kumudu gharama za matibabu na hivyo kuomba serikali
kusimamia kumaliza migogoro hiyo.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Mabwegere Mika Kashu amekiri baadhi ya
wanawake kuishi katika mazingira magumu ambapo amesema waliohusika na
mauaji hayo wanafahamika na hivyo kuomba serikali iwachukulie hatua
kwani oparation ya kamatama imesababisha hofu na wanaume kulazimika
kukimbia kijiji.
Afisa utawala wa wilaya ya Kilosa Hilary Sagala akizungumza na kwa anjia ya simu amesema jeshi la polisi limeimarisha ulinzi katika
eneo la Mabwegere na kuhusu wafugaji kukimbia makazi amesema hakuna
sababu ya watu kukimbia makazi kama hawakuhusika na tukio la
lililosababisha mauaji na kuwataka wananchi kurejea katika makazi yao
waendelee na shughulizao kama kawaida.
Social Plugin