Moja kati ya matatizo yanayowakumba watu wengi kwa kizazi cha sasa ni
tatizo la uzito , tatuizo hili limekuwa chanzo cha matatizo mengine
makubwa na yenye madhara makubwa kwa afya ambayo wakati mwingine
husababisha kifo .
Magonjwa ya moyo , kisukari , shinikio la damu la kupanda na kushuka ,
nguvu za kiume , matatizo ya figo na viungo vingine vya mwili pamoja na
kukosa mvuto wa kawaida yanasabishwa na mtu kuwa na uzito ambao
anashindwa kuumudu .
Uzito huongezeka kutokana na mtindo Fulani wa maisha ya mwanadamu na
pia unaweza kupungua kutokana na mtindo huu huu wa maisha ambao kama
ukimudu kuuzingatia hasa kwenye chakula unaweza kupungua uzito na kuishi
maisha kwa raha na kwa afya salama .
Ifuatayo ni orodha ya vyakula vya aina nne tofauti ambavyo unaweza
kuanza kuvipanga kwenye chakula chako ambavyo visaidia sana kupungua
uzito .
1.Mayai Mazima
Katika miaka ya hivi karibuni tafiti nyingi ambazo si sahihi na si za
kweli zimesababisha watu kutozingatia ulaji wa mayai hasa yakiwa mazima
na muhimu kuliko yote ni ile sehemu ya kiini cha yai .
Watu wengi
wameaminishwa kuwa kiini cha yai kina mafuta ambayo ulaji wake huweza
kufanya mtu anenepe bila mpangilio.
Mafuta yanayopatikana kwenye kiini cha yai si mafuta mabaya bali ni
yale amabyo mwili inayahitaji na hayana hatari kwa mwili wa binadamu .
Kiini cha yai kina virutubisho muhimu sana kwa mwili wa mwanadamu
ikiwemo protini pamoja na chembechembe zinazosaidia kupunguza sumu
mwilini .
2.Chokoleti Nyeusi .
Tafiti nyingine zisizo sahihi zimewaaminisha wengi kuwa chokoleti sio
kitu kizuri , lakini ni kinyume chake kwani si kila chokoleti zina
madhara kwa mwanadamu na baadhi yake ikiwemo zile nyeusi zina faida
kubwa mwilini .
Asilimia 70 ya chembechembe zinazotengeneza chokoleti nyeusi ni kokoa
, chokoleti hii ina virutubisho pamoja na madini muhimu mwilini kama
vile Magnesium pamoja na manganese ambayo husaidia mwili katika masuala
mbalimbali ikwiemo kuponya vidonda na kuridishia chembechembe hai za
mwili zinazopotea .
Chokoleti nyeusi pia husaidia kupunguza uwezekano wa mtu kupata
maradhi ya moyo na maradhi mengine yatokanyo na shinikizo la damu .
3.Samaki Wadogo ‘Dagaa’.
Samaki wadogo ambao hufahamika kama dagaa wana faida nyingi sana
mwilini , sababu kubwa ya faida yao ni jinsi amabvyo wanaliwa wazima kwa
maana ya ngozi yao , mifupa na vitu vyote vilivyomo ndani yake ambavyo
kimsing vina faida kubwa sana .
Dagaa wana kila kitu ambacho mwili wa mwanadamu unahitaji kwa maana
ya virutubisho ambavyo vinaboresha afya na kumpa mtu nguvu pamoja na
kinga dhidi ya magonjwa na pia kusaidia kuponya magonjwa pale mtu
anapokuwa mgonjwa .
- Nyama ya Ini .
Katika hali ya kawaida ile kauli ya kusema kuwa nyama nyekundu si
nzuri kwa mwanadamu ina usahihi wake na ina mahali ambako si sahihi .
Usahihi wake ni kwamba , nyama nyekundu si nzuri kwa mwili wa
mwanadamu . Lakini kuishia hapo ndio mahali ambako kauli hii inacha kuwa
sahihi , kwani ukweli ni si nyama zote nyekundu si nzuri kwa mwanadamu
kuna nyama ambazo ni sahihi na nyingine si sahihi .
Nyama ya ng’ombe na
mbuzi zina madhara makubwa zinapoliwa kwa wingi na pasipo mpangilio .
Lakini kuna nyama nyekundu ambazo zinahitajika mwilini na mojawapo kati ya nyama hizi ni nyama ya ini .
Hata wanyama kwa mfano simba wanafahamu hili na ndio maana Simba
anapoua mnyama huanza kula viungo vyake vy andani kabla ya kula sehemu
nyingine .
Nyama ya ini virutbisho muhimu kama vile Vitami A , madini mbalimbali
kama Shaba , Zinc , Selenium , Folate na Niacin pamoja na Protini kwa
kiwango kikubwa sana .
Virutubisho vyote hivi vina faida kubwa sana
mwilini mwa mwanadamu . Kula nyama ya ini hata mara moja kwa wiki ina
faida kubwa sana .
Social Plugin