Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Liberatus Sangu kutoka Jimbo Katoliki la Sumbawanga, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Tanzania.
Kabla ya uteuzi wake, Askofu mteule Sangu alikuwa ni Afisa
mwandamizi katika Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu mjini
Vatican.
Askofu mteule Liberatus Sangu alizaliwa tarehe 19 Februari 1963, Kijijini Mwanzye, Jimbo Katoliki la Sumbawanga.
Askofu mteule Liberatus Sangu alizaliwa tarehe 19 Februari 1963, Kijijini Mwanzye, Jimbo Katoliki la Sumbawanga.
Baada ya
masomo na majiundo yake ya kikasisi kwenye Seminari kuu la Kibosho,
Jimbo Katoliki Moshi na Segerea, Jimbo kuu la Dar es Salaam,
akapadrishwa kunako tarehe 9 Julai 1994.
Katika maisha yake kama Padre, Askofu mteule Sangu amewahi kuwa Mlezi wa Seminari ndogo ya Kaengesa, Jimbo Katoliki la Sumbawanga kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 1995.
Katika maisha yake kama Padre, Askofu mteule Sangu amewahi kuwa Mlezi wa Seminari ndogo ya Kaengesa, Jimbo Katoliki la Sumbawanga kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 1995.
Akateuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya Matai kuanzia mwaka 1995 hadi
mwaka 1996.
Kati ya Mwaka 1996 hadi mwaka 1999 alikuwa mjini Roma kwa
masomo ya juu na kujipatia shahada ya Uzamili katika taalimungu ya
Sakramenti za Kanisa, kutoka katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu
Anselmi, kilichoko mjini Roma.
Kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2000, aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Parokia ya Mwanzye.
Kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2000, aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Parokia ya Mwanzye.
Kuanzia mwaka
2000 hadi mwaka 2007 akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa miito Jimbo
Katoliki la Sumbawanga; mlezi katika mwaka wa malezi na mkurugenzi wa
utume wa vijana, Jimbo Katoliki Sumbawanga.
Kunako mwaka 2007 hadi mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Paroko wa muda Parokiani Sopa.
Kunako mwaka 2007 hadi mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Paroko wa muda Parokiani Sopa.
Kuanzia mwaka 2008
hadi uteuzi wake, amekuwa akitekeleza utume wake kama Afisa mwandamizi,
Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu mjini Vatican.
Itakumbukwa kwamba, Jimbo Katoliki la Shinyanga, Tanzania kuanzia mwaka 2012 limekuwa wazi kufuatia kifo cha Askofu Aloysius Balina.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.