Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Ilola
iliyopo katika wilaya ya Shinyanga vijijini aitwaye Veronica Venance mwenye
umri wa miaka 12 amefariki dunia kwa kupigwa na mwanafunzi mwenzake wakati
wakigombania daftari darasani kwa ajili ya kuandika notes.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea Februari 24
mwaka huu, saa 7 na nusu mchana katika
darasa la tano shule ya msingi Ilola iliyopo katika kata ya Ilola tarafa ya Itwangi
wilaya ya Shinyanga.
Mshuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa mwanafunzi huyo amefariki
dunia baada ya kupigwa makofi na ngumi sehemu za kichwani na mwanafunzi
mwenzake aitwaye Sophia Mathew(12).
Social Plugin