Mzee Samwel Lupilya (62) mkazi wa kitongoji cha Madukani kijiji
cha Sakwe wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu anayesumbuliwa na kansa tangu mwaka
jana.
Anasema alikwenda hospitali ya wilaya ya Bariadi ambayo sasa
ni hospitali ya mkoa wa Simiyu ambapo aliambiwa na madaktari kuwa ugonjwa
unaomsumbua unatibiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Kama anavyoonekana pichani upande wa kulia wa uso,shingoni
na kuna kidonda kikubwa sasa kuonekana kusambaa sehemu za mwili wake na
kumsababishia maumivu makali.
Anasema baada ya kufika Bugando aliambiwa na wahusika wa hospitali hiyo kutoa shilingi
Milioni moja na laki 6 kwa ajili ya matibabu ,pesa ambazo alidai hana
akalazimika kurudi nyumbani kusubiri msaada kutoka wasamaria wema huku
akionekana kukata tamaa ya kuishi.
Kama umeguswa na ugonjwa wa mzee huyu piga simu namba
0768140069 kwa ajili ya mchango wako
Social Plugin