Siku tatu tu baada ya watu watatu kuuawa kwa kukatwa mapanga
kisha kufungiwa ndani ya nyumba zaidi ya siku 5 katika kijiji cha Bugogo wilaya
ya Shinyanga,mauaji ya watu wa kukatwa mapanga yameendelea kujitokeza ambapo
huko katika kijiji cha Manyada,kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga mwanamke mmoja
ameuawa kwa kukatwa mapanga akiwa amelala nyumbani kwake.
Tukio hilo limetokea jana saa nane usiku.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha(pichani) amemtaja aliyeuawa kuwa ni Winifrida
Simon(35) ambaye alivamiwa akiwa amelala ndani ya nyumba yake na watu
wasiofahamika kisha kukatwa mapanga kichwani na shingoni.
Amesema chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa na kwamba
tayari watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Kamanda Kamugisha amewataja wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni
Misana Juma(30),Joseph Jahila(24) Emmanuel Joseph(39) na Msafiri Kulwa wote
wakazi wa Manyada kata ya Usanda tarafa ya Samuye wilaya ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Social Plugin