Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMBAZI LAKAMATWA NA RISASI 166 NA BUNDUKI HUKO KAHAMA

 
 Vitu alivyokutwa navyo

Risasi 166 alizokutwa nazo jambazi huyo
Mtuhumiwa
Mwanamme mmoja anayedaiwa kuwa jambazi aliyejulikana kwa jina la Saidi Maulidi (35) mkazi wa Mulubona wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma amekamatwa na risasi 166 akiwa na risasi hizo na bunduki aina G3LMG pamoja na makoti mawili ndani ya basi alilokuwa anasafiri nalo.



Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Busoka  wilayani kahama mkoani Shinyanga jana majira ya jioni,akiwa anatokea mkoa wa Kigoma kuelekea mkoa wa Singida.



Kwa mujibu wa  mashuhunda wa tukio hilo walisema kuwa jambazi hilo likuwa kwenye basi la abiria la Bariadi Express lililokuwa likitokea mkoani Kigoma na baada yaa kumshtukia abiria walitoa taarifa kwa askari wa doria ambao walilisimamisha basi hilo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema jambazi hilo lilikuwa kwenye  basi la Bariadi Express aina ya Scania lenye namba T186 BFY.



Kamanda Kamugisha alisema jambazi hilo lilikuwa vitu vingine kama vile,makoti mawili ambayo yanafanana makoti ya kipolisi.



Kamungisha aliwaomba abiria na raia wema kuwa na ushirikiano na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa kwani ni wajibu wa kila mwananchi kutumia nafasi ya kutoa tarifa.



Kamanda Justus amesema kuwa jeshi hilo la polisi linamshikilia mhutumiwa huyo na uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika atafikishwa mahakamanni kujibu tuhuma zinazomkabili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com