NB- Picha haihusiani na Habari hapa chini |
MCHUMI wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Brown Kajange (42) amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo jijini Dar es salaam kujibu mashitaka mawili, likiwamo la shambulio la aibu kwa kumshika matiti mwanamke bila ridhaa yake.
Karani
wa Mahakama hiyo, Blanka Shao alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu
Matrona Luanda kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari 16, mwaka huu
katika eneo la kuuzia samaki la Feri Kivukoni wilaya ya Ilala.
Shao
alidai siku ya tukio saa 6 mchana katika eneo hilo, mshtakiwa alimshika
matiti Queensia Fusi bila ridhaa yake huku akijua kufanya hivyo ni
kinyume cha sheria.
Alidai
kuwa shtaka la pili, mshtakiwa alimpiga ngumi mlalamikaji katika jicho
la kushoto na kusababisha maumivu makali katika sehemu hiyo.
Mshtakiwa
alikana mashtaka na Hakimu Luanda aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 3,
mwaka huu itakapotajwa.
Mshtakiwa
yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na
mdhamini mmoja mwenye barua kutoka serikali ya mtaa, atakayesaini bondi
ya Sh 300,000.
Social Plugin