Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIJANA AJIUA KWA KUJICHINJA KWA PANGA AKIWA CHOONI HUKO GEITA

NB-Picha haihusiani na habari hapa chini
Kijana mmoja mkazi wa mtaa wa Lwenge mjini Geita Stephen Singa(36) amekutwa amejichinja mwenyewe kwenye koromeo kwa kutumia panga na kufa hapo hapo akiwa chooni.

 
Tukio hilo limetokea leo mchana saa saba ambapo kaka wa marehemu Ogola Joel ameiambia Malunde1 blog kuwa amepata taarifa hizo mchana akiwa kazini kwake.

Amesema alipofika nyumbani amekuta marehemu akiwa chooni amekufa huku chanzo chake kikiwa hakijafahamika na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya Geita.
Kamanda wa polisi  mkoa wa Geita Joseph Konyo alipotafutwa kwa njia ya simu hakuweza kupatikana ili  kuongelea tukio hilo.
Na Valence Robert- Malunde1 blog Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com