Mkazi wa Tabata, Erasto Clement (22) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kukana mashitaka ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 16.
Akisomewa
maelezo ya awali jana, Wakili wa Serikali Felista Mosha alidai mbele ya
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan kuwa katika tarehe na mwezi
usiofahamika, mwaka jana, Clement pamoja na mlalamikaji walidaiwa kuwa
wanafahamiana kwa muda mrefu.
Mosha
alidai kuwa Septemba, 2013 mshitakiwa na mlalamikaji walianza mahusiano
ya kimapenzi na kumuingilia kimwili mlalamikaji huyo huku akijua
kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
Pia alieleza kuwa mlalamikaji aliripoti taarifa hizo katika kituo cha Polisi na kupewa PF3 kwa ajili ya kwenda hospitali.
Wakili Mosha alidai kuwa mlalamikaji alipofika hospitali alipimwa na kukutwa na ujauzito wa miezi sita.
Mshitakiwa alikubali maelezo yake binafsi pia alikana kufikishwa mahakamani hapo kusomewa mashitaka yanayomkabili.
Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulidai kuwa utakuwa na mashahidi wanne na kielelezo kimoja ambacho ni PF3.
Hakimu Hassan aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili Mosi mwaka huu itakapoanza kusikilizwa.
Social Plugin