ITV imeshuhudia msafara wa magari ya kijeshi pamoja na yale ya
maofisa wa kijeshi na huduma ya kwanza yakipita katika barabara kuu
itokayo Tanga kwenda Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania kisha
kuingia katika njia iendayo katika mapango yaliyodaiwa kuwa ni sehemu
maalum ya maficho ya vikundi hivyo vya kigaidi na msemaji wa polisi
kamishna wa polisi -operesheni Paul Chagonja kutwa nzima simu yake
iliita bila majibu lakini msaidizi wake alipoke na kudai kuwa bosi wake
yupo kwenye kikao.
Hata hivyo baadhi ya familia zilizopo katika eneo la Mleni
zinadaiwa kuhamisha makazi kufuatia milipuko ya risasi na silaha nzito
za kijeshi zilizokuwa zikirindima katika kipindi cha siku mbili nyakati
za mchana na usiku, hatua ambayo baadhi ya makundi ya vijana
yanaojihusisha na kazi ya kupasua mawe katika mapango hayo kulalamikia
ukosefu wa kazi kwa sababu ya mapigano hayo ambayo pia yamewapa hofu na
maisha yao.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wameshauri mapango hayo
yaharibiwe kwa kutumia vifaa maalum vya kivita na jeshi la polisi
lisahau suala la silaha zao zilizoibwa katika matukio tofauti na makundi
hayo.
Via>>ITV
Social Plugin